Suluhisho la ugaidi wa kimataifa ni mjadala-Mhadhiri.

2 Julai 2018

Nguvu za kupindukia za kijeshi hazitamaliza ugaidi duniani na badala yake mazungumzo ndio mwelekeo sahihi wa kuleta maelewano.

Dkt. Kiggundu Muhammed Musoke ambaye ni mhadhiri wa Chuo  Kikuu cha Makerere nchini Uganda amesema hayo akihojiwa na Idhaa hii jijini New York Marekani alikokuwepo kwa ajili ya mkutano wa masuala ya ugaidi na misimamo mikali ya kidini.

Ametoa mfano wa mbinu za kijeshi zitumiwazo hivi sasa na mataifa mengi kukabiliana na ugaidi

(SAUTI YA KIGGUNDU )

 Mbali na hayo  inasemekana vijana wengi wanaojitosa katika ugaidi hupatiwa fedha ambazo ndio wanatafuta.

(SAUTI YA KIGGUNDU )

Dkt Kiggundu ambaye pia anawakilisha asasi ya kiraia  ya Muslim Centre for Justice and Law ya nchini Uganda akaelezea alichozungumzia kwenye mkutano huo wa masuala ya ugaidi.

(SAUTI YA KIGGUNDU)

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud