Ugaidi unasalia kuwa tishio kubwa duniani, mshimakamano ni dawa mujarabu: INTERPOL

29 Juni 2018

Ugaidi unasalia kuwa tishio kubwa la maisha ya watu na miundombinu duniani na Umoja wa Mataifa mjini New York unalitambua hilo ndio maana juma hili umeitisha mkutano wa ngazi ya juu uliotoa kipaumbele kwa suala hili.

Maaafisa wa mashirika ya kupambana na ugaidi kutoka nchi wanachama , mashirika wadau na Umoja wa Mataifa wamehudhuria mkutano huo unaokunja jamvi leo, lengo likiwa kutafuta dawa mujarabu ya hofu iliyotanda ya uwezo wa magaidi kusambaratisha mifumo muhimu ya jamii kama vile ya nishati, bank, intaneti na kadhalika.

Moja ya mashirika muhimu yaliyoshiriki mkutano huo ni INTERPOL shirika la polisi wa kimataifa wa kupambana na uhalifu ambalo linachagiza ushirikiano miongoni mwa majeshi ya polisi kote duniani kupambana na zahma hii.

Katibu Mkuu wa  INTERPOL ni Jürgen Stock,    anasema ugaidi ni mtihani wa kimataifa na mtu au taifa moja pekee haliwezi kuushinda ndio maana shirika lake limeshiriki mkutano huu ambao ni

(SAUTI YA JURGEN STOCK-1)

Wa kuhusu kubadilishana uzoefu, kushirikiana ujuzi, na hatimaye kufanya mtandao wetu wa kimataifa dhidi ya uhalifu kuwa imara zaidi na cha muhimu kabisa ni kupeana taarifa muhimu ambazo zinahitajika na polisi kwa sababu magaidi na wahalifu bila shaka wanafaidika na utandawazi.”

 

CITES inasaidia operesheni za INERPOL za kuwasaka na kuwakamata wahalifu waliotoroka ( INFRA-Terra) kwa makosa ya uhalifu wa mazingira hususani uhalifu dhidi ya wanyamapori
PICHA: INTERPOL/CITES
CITES inasaidia operesheni za INERPOL za kuwasaka na kuwakamata wahalifu waliotoroka ( INFRA-Terra) kwa makosa ya uhalifu wa mazingira hususani uhalifu dhidi ya wanyamapori

Amesema ingawa kuna changamoto katika vita hivi juhudi za kila njia zinafanyika kuubabili ugaidi kwa sasa mfano

(SAUTI YA JURGEN STOCK-2)

Tuna mfumo bora wa kimataifa wa mawasiliano ambao unaitwa i-24/7 ambao unawaunganisha maafisa wa polisi kutoka nchi wanachama 192, kote duniani na unatoa jukwaa ambalo linaungwa mkono na Umoja wa Mataifa , kupitia maazimio ya baraza kuu na maazimio kadhaa ya baraza la usalama yanazichagiza nchi wanachama kutumia uwezo huu unaotolewa na INTERPOL . Tunaendesha kanzi data 17 (data base) kubaini magaidi na wahalifu lakini taarifa hizi zinahitaji kuwafikia polisi hivyo tunaunda mfumo wa kimataifa wa kutoa tahadhari mapema dhidi ya ugaidi na uhalifu wa kupangwa.”

Kisha Bwana Stock akatoa wito

(SAUTI YA JURGEN STOCK -3)

“Nadhani kila mtu anajukumu la kufanya  kwani ni changamoto ya kijamii kwa hakika, kalini kwanza cha msingi ni kuendelea na maisha ya kawaida , pili ni muhimu kuongeza kiwango cha uelewa , ukiona kitu kinakutia shuku basi toa taarifa kwa polisi kuhusu shuku hiyo, pia kuzuia itikadi kali, kuzuia watu kuingia katika kazi za itikadi kali, haya yanahitaji mtazamo wa pamoja, juhudi za asasi za kiraia, vyombo vya dola, hata bodi za elimu pia zina jukumu, inahitaji mkakati maalumu na imara katika ngazi zote , ya taifa na kimataifa.”

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter