Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita dhidi ya ugaidi yashika kasi mashinani Kenya- VITOK

Baadhi ya washiriki wa kongamano la kupambana na ugaidi lililoandaliwa na shirika la waathirika wa ugaidi nchini Kenya, VITOK huko kaunti ya Kakamega nchini Kenya.
VITOK
Baadhi ya washiriki wa kongamano la kupambana na ugaidi lililoandaliwa na shirika la waathirika wa ugaidi nchini Kenya, VITOK huko kaunti ya Kakamega nchini Kenya.

Vita dhidi ya ugaidi yashika kasi mashinani Kenya- VITOK

Amani na Usalama

Harakati zinaendelea ili kuhakikisha jamii ya kimataifa pamoja na serikali zinashirikiana kukabiliana na ugaidi ambao ni mwiba hivi sasa duniani.

Kila uchao, magaidi wa kitaifa na kimataifa wanaibuka na mbinu mpya, vivyo hivyo tunapaswa kusaka mbinu mpya za kukabili vitendo hivyo viovu, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati akifungua kikao cha ngazi ya juu chenye lengo la kukabili ugaidi duniani. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta Massoi)

Mkutano huo wa siku mbili, wa kwanza wa aina yake unafanyika jijini New York, Marekani ambapo Katibu Mkuu ametaja malengo sita ya kuzingatia ili kuondokana na ugaidi ambao unaathiri kila nchi hivi sasa.

Malengo hayo ni pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, kuzingatia haki za binadamu katika kukabili ugaidi na kuwa na uwekezaji wa kimkakati kwa vijana ili wasitumbukie kwenye ugaidi na misimamo mikali.

Image
Kitabu cha mwongozo wa uandishi wa habari za ugaidi. Picha: UNESCO

Nchini Kenya, shirika la kiraia la wahanga wa kigaidi, VITOK tayari limechukua hatua ikiwemo kuandaa kongamano huko Kaunti ya Kakamega ambapo Mkurugenzi wake James Ndeda anasema lilijumuisha mafunzo…

(Sauti ya James Ndeda)

Na kutokana na kongamano hilo wanaandaa kitabu cha mafunzo kwa wahamasishaji dhidi ya ugaidi kikijumuisha mambo kadhaa ikiwemo…

(Sauti ya James Ndeda)