Bado haki za binadamu zinakiukwa Eritrea:Keetharuth

Watoto wakiwa mji wa Embetyo nchini Eritrea
OCHA/Gemma Connell
Watoto wakiwa mji wa Embetyo nchini Eritrea

Bado haki za binadamu zinakiukwa Eritrea:Keetharuth

Haki za binadamu

Mtaalamu maalum wa umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu  nchini  Eritrea,  ameelezea wasiwasi wake kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo pamoja na mvutano wa mpaka unaondelea kati ya Eritrea na jirani yake Ethiopia.

Akitoa ripoti yake ya tano na ya mwisho  kwa baraza la haki za binadamu mjini Geneva Uswisi hi leo, Bi. Sheila Keetharuth, amesema hofu yake ni kwamba visa vya ukiukwji wa haki za binadamu ambavyo vimekuwa vikiorodheshwa tangu miaka humo miaka sita iliyopita nchini humobado vinaendelea.

Ameongeza kuwa ameshindwa kutoa tarifa zozote za maendeleo ya haki za binadamu tangu alizozuru nchini humo mara kwanza , kwa sababu hakuna mabadiliko yoyote licha ya wito kutoka Umoja wa Mataifa, baraza la haki za binadamu na wadau wengine wanaotaka kuona mabadiliko ya haki nchini humo.

Bi Keetharuth ametaja baadhi ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Eritrea ni pamoja na  watu kukamatwa, kuswekwa rumande kiholea, kushurutishwa kuingia jeshini na kupigwa marufuku kwa haki kadhaa za msingi.

kuwakamata watu na kuwaweka ndani kiholela, utumikishwaji jeshini wa lazima pamoja na marufuku kadhaa  kuhusu haki za kimsingi.

 Amesisitiza kuwa hali hiyo haikubaliki  huku serikali imeonyesha kujikokota katika hatua za kuhakikisha inashughulikia  itashughulikia visa hivyo. Amesema ni muhimu kwa mustakhbali wa taifa hilo kuhakikisha suluhu ya hali hiyo inapatikana

 Kwa upande wa mvutano wa mpaka baina ya Eritrea na Ethiopia  amesema 

Image
Sheila B. Keetharuth, Mratibu Maalum kuhusu haki za binadamu Eritrea. Picha ya UN/Jean Marc Ferré.

 

(SAUTI YA SHEILA KEETHARUTH)

 “Mimi na tume ya uchunguzi, mara kadhaa  tumetaka utekelezwaji wa  uamuzi wa mwaka 2002 wa tume ya mpaka kati ya Eritrea na Ethiopia. Kwa upande huo nakaribisha  juhudi za hivi majuzi za kufikia muafaka kwa njia ya amani kati ya Eritrea na Ethiopia.”

 Pamoja na hatua hiyo nzuri ya mvutano wa mpaka ametoa wito kwa serikali kuunda taasisi madhubuti zenye msingi wa utawala wa sheria na mahakama iliyo huru, kuwa na bunge ambalo limechaguliwa kidemokrasia, kutoa fursa kwa vyama vya kisiasa vyenye mitazamo tofauti na kuwa na vyombo vya habari  vilivyo huru.”

Nayo Eritrea kwa upande wake , imesema imekuwa ikidhalilishwa na wajibu na baraza hilo la haki za binadamu na kwamba ripoti hiyo haijachagizwa na hofu ya haki za binadamu bali na malengo ya kisiasa ya kutaka kuitenga Eritrea kwamba ina kiuka haki za binadamu. Eritrea imeikataa ripoti hiyo na kuanzisha rufaa ya kutaka baraza la haki za binadamu kuacha kuidhalilisha na kuanza mazungumzo kwa kuzingatia kanuni.