Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hukumu ya miaka 5 jela dhidi ya Wangchuk China si haki:UN

Kikao cha Baraza la haki za binadamu. (Picha:OHCHR/Facebook)

Hukumu ya miaka 5 jela dhidi ya Wangchuk China si haki:UN

Haki za binadamu

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamesema hukumu ya miaka mitano jela iliyotolewa dhidi ya mwanaharakati wa haki za binadamu wa Tibet Tachi Wangchuk nchini China si haki.

Wataalamu hao 6 wanaohusika na masuala ya haki dhidi ya mifumo ya ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni na kutovumilina, haki za utamaduni, haki za walio wachache, haki za watu kutoshikiliwa kiholela na kuchagiza na kulinda uhuru wa maoni na kujieleza, wamelaani vikali hukumu hiyo iliyotolewa na mahakama ya Uchina.

Tashi Wangchuk mwanaharakati wa kuchagiza haki za utamaduni na lugha ya Watibet walio wachache nchini Uchina alikamatwa Januari 2016 kwa kushiriki katika makala ambapo alitoa wito wa kutolewa elimu kwa lugha ya wachache ya Kitibet na kuwepo kwa haki ya watu wa Tibet  kushiriki maisha yao ya kitamaduni.

Tangu alipokamatwa Wangchuk amekuwa akikishikiliwa rumande, lakini sasa mahakama ya China imemkuta na hatia ya kuchochea kujitenga na hivyo kumkatia kifungo hicho cha miaka mitano jela.

Watalaamu hao wa Umoja wa Mataifa wanasema hatua hiyo ni kujaribu kunyamazisha wanaharakati wa haki za binadamu na ni suala lisilokubalika.

TAGS: China, Tibet, Haki za binadamu, Tashi Wangchuk