Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua ya wagombea urais Colombia ni ya kuigwa:Zeid

Waliokuwa wapiganaji wa FARC wakiwa kwenye mazungumzo na viongozi wa kijami nchini Colombia kama njia ya kujumuishwa tena kwenye jamii.Htua hiyo imewezesha kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini humo
Jennifer Moreno/UN Verification Mission
Waliokuwa wapiganaji wa FARC wakiwa kwenye mazungumzo na viongozi wa kijami nchini Colombia kama njia ya kujumuishwa tena kwenye jamii.Htua hiyo imewezesha kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini humo

Hatua ya wagombea urais Colombia ni ya kuigwa:Zeid

Amani na Usalama

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa , Zeid Ra'ad Al Hussein amepongeza hatua ya wagombea kiti cha urais nchini Colombia ya kuapa kuheshimu , kulinda na kuhakikisha haki za binadamu endapo wakichaguliwa na kukiita ni kitendo cha  kuvutia na kisicho na kifani.

Wagombea hao watano wa kiti cha urais wametia saini makubaliano kuwa wataheshimu na kulinda haki za binadamu endapo mmoja wao atachaguliwa kuliongoza taifa hilo katika uchaguzi mkuu wa Jumamosi (Leo)

 "Tunaamini hii ndiyo mara ya kwanza kuwahi kufanyika popote pale kuwa kila mgombea kiti cha urais kutia sahihi ahadi ya kudumisha haki za binadamu," amesema Zeid. " Na kuongeza kuwa hii inaleta mwamko mpya duniani ambako viongozi wa kisiasa wengi wamekuwa wakidharau ama kupuuza  wajibu wao wa kudumisha sheria za kimataifa za haki za binadamu.

Amewashukuru viongozi hao wa Colombia kwa kuchukua hatua hii  yenye kuleta matumaini na kumhimiza yeyote atakaeibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu ahakikishe kuwa anafanya kila juhudi kufuata makubaliano haya.

 Katika tarifa yake Zeid amesema mkataba kuhusu haki za binadamu, ulioandaliwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu nchini Colombia na kutiwa saini na kila mmoja wao unasema hivi:

 Mimi, kama mgombea kiti cha urais wa Jamhuri ya Colombia, naapa hadharani kuwa, katika serikali yangu, kutakuwa na mkazo maalum wa kuheshimu, kulinda na kuhakikisha haki za binadamu.

 

"Wakati huohuo,vitendo vya serikali yangu vitaendeleza nchini kote na hususan katika maeneo ambayo yameathirika mno na migogoro pamoja na ghasia, kuwahusisha watu wa maeneo hayo katika  masuala ya kisiasa,kiuchumi na kijamii."

Katika kutambua matatazo mengi yanayoisumbua nchi hiyo, Zeid amesema mkataba huo pia unabaini tathmini ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, na kusisitiza kuwa "ni muhimu kuepuka hatua ya kuwaua viongozi, wawe wa sehemu za mashambani pamoja na watetezi wa haki za binadamu jambo litachangia kufikia hali halisi ya kuwajumuisha katika nchi hiyo kisiasa, kijamii na kiuchumi,".

Wakati wa kutangaza mkataba huo mjini Bogota siku ya Alhamisi,mjumbe wa  ofisi ya haki za bindamu ya Umoja wa Mataifa nchini Colombia, Alberto Brunori aligusia changamoto kubwa nne zitakazomkabili rais mpya ambazo ni:

1- Kukabilina na ukwepaji wa sheria pamoja na kesi za mauaji ya wanawake;

2-Kutoa ulinzi kwa watetezi wa haki za binadamu jambo ambalo limekuwa mwiba nchini humo;

3-Kutumia nafasi hii, ilioletwa na mchakato wa amani, kuimarisha  dola linaloheshimu haki za binadamu kupitia taasisi za mashinani;

4 – Na kutoa ulinzi wakati wakiheshimu haki za binadamu.

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa , Zeid Ra'ad Al Hussein
Picha ya UN/Jean-Marc Ferré
Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa , Zeid Ra'ad Al Hussein

 

Akisema kuwa changamoto hizo zimekuwa kikwazo cha maendeleo ya kisiasia, kijamii na kiuchumu nchini  Colombia. Zeid ameongeza kuwa mojaya hatua moja mbele ni hatua ya wagobea wote watano kuapa kuheshimu haki hizo.

"Mimi na wafanyakazi wangu, na watu wote wa Colombia, tunamatumaini kuwa kila mara watakuwa wanamkumbusha  atakaechaguliwa kuhusu hilo.Kuapa ni jambo moja na kutimiza ni jingine." amesema.