Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda acheni kuwakamata wapinzani wa kisiasa kabla ya uchaguzi:UN

Kutoka Maktaba: Abiria akiwa kwenye usafiri wa pikipiki maarufu kama Boda Boda mjini Kampaka nchini Uganda
© World Bank/Sarah Farhat
Kutoka Maktaba: Abiria akiwa kwenye usafiri wa pikipiki maarufu kama Boda Boda mjini Kampaka nchini Uganda

Uganda acheni kuwakamata wapinzani wa kisiasa kabla ya uchaguzi:UN

Haki za binadamu

Wataalam huru wa hali za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo wametoa wito kwa mamlaka ya Uganda kukomesha vitendo vya kuwakamata, kuwasweka rumande na kuwadhalilisha wapinzani wa kisiasa, viongozi wa asasi za kiraia na watetezi wa haki za binadamu.

Wito huo uliotolewa leo Jumanne umekuja wakati ambapo machafuko yameshika kasi kabla ya uchaguzi mkuu war ais uliopangwa kufanyika Januari 14 huku kukiwa na ripoti za kifo cha mlinzi wa kiongozi wa upinzani na waandishi watatu wa Habari kujeruhiwa baada ya kupigwa mabomu ya machozi Jumapili.

“Tunatiwa hofu kubwa na mchafuko yanayohusiana na uchaguzi, matumizi ya nguvu kupita kiasi yanayotekelerzwa na watu wa ulinzi Pamoja na kuongezeka kwa msako dhidi ya watu wanaoandamana kwa njia ya amani, viongozi wa kisiasa na wa asasi za kiraia na watetezi wa haki za binadamu.”mesema wataalam hao.

Kundi la wataalam hao pia limerejea kuelerzea hofu zao katika matumizi mabaya na ukiukaji wa vikwazo vya kiafya nchini humo kabla ya uchaguzi mkuu.

“Kila mara tumekuwa tukisisitiza kwamba vita dhidi ya janga la coronavirus">COVID-19 vitumike kama kigezo cha kubinya uhuru wa msingi wa watu. Kupambana na ugaidi pia kusitumike kama halalisho la kukandamiza uhalali wa masuala mbalimbali au kuzuia kazi na masuala yah alali.”

Ombi kwa mamlaka

Wataalam hao huru wa Umoja wa Mataifa wameitaka malaka nchini Uganda kufuta madai yote dhidi ya wale ambao wamekamatwa wakati wa kipindi cha kampeni za uchaguzi na kumaliza mara moja vitisho vya kisheria dhidi ya watetezi wa haki za binadamu, waandishi wa Habari, viongozi wa asasi za kiraia , watu wanaoandamana kwa amani, vyama vya kisiasa na wale ambao wanaonyesha mtazamo tofauti au kuasi.

“Tunaonya dhidi yah atua zinazochukuliwa na polisi na mfumo wa haki na sheria ambayo vinaweza kuwa na athari mbaya katika maeneo ya kijamii katika kuelekea uchaguzi huu mkubwa”imeendelea kusema taarifa yao na kuongeza kwamba“Vitendo hivyo vinaweza kuzusha hofu na kuvunja moyo kampeni ambazo ni za wazi na pia uchaguzi huru na wa haki.”

Wataalam hao wametoa wito kwa serikali ya Uganda kuchukua hatua zote za lazima kuhakikisha mazingira salama kwa ajili ya kufanyika uchaguzi wa amani, huru na wa uwazi.

Wakihitisha taarifa yao wataalam hao wamesisitiza kwamba“Hatua zozote zinazoweza kuchochea mivutano zaidi ya kijamii lazima ziepukwe, na sauti za wat una wawakilishi lazima zipewe uzito.”