Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS yaimarisha ulinzi kwa raia jimboni Unity

Ghasia zinashuhudiwa katika jimbo la Unity nchini Sudan Kusini.
UNMISS/Eric Kanalstein
Ghasia zinashuhudiwa katika jimbo la Unity nchini Sudan Kusini.

UNMISS yaimarisha ulinzi kwa raia jimboni Unity

Amani na Usalama

Takriban walinda amani 150 leo wamepelekwa haraka kwenye jimbo la Unity nchini Sidan Kusini katika jitihada za mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNMISS, ili kuwalinda raia ambao wanalengwa kwa maksudi na pande kinzani katika mzozo unaonendelea.

Akizungumzia umuhimu wa kufanya hivyo mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Sudan kusini na Mkuu wa UNMISS David Shearer amesema

(SAUTI YA DAVID SHEARER )

Tunachokishuhudia ni mauaji ya makusudi ya raia, ubakaji na kutekwa kwa wanawake na watoto, nyumba na maisha ya watu kusambaratishwa katika njia ambayo inazuia familia kujerea kwenye makazi yao na kuweza kujikimu.”

Ameongeza kuwa maelfu ya raia wanakimbia mapigano wakati huu ambapo makundi yenye silaha yakijongea kutoka eneo la Koch kuelekea mji wa Leer. Takriban vijiji 30 au makazi yameshambuliwa.

UNMISS na timu ya haki za binadamu wameshuhudia maiti za raia waliouawa wakati wa mapigano zikiwa zimezagaa mitaani bila kuzikwa, nyumba nyingi zikiwa zimechomwa, wizi wa ng’ombe, na kusambaratishwa kwa huduma muhimu kama visima vya maji, vituo vya afya na maghala ya chakula.  Amesema hali hii haikubaliki kwani

(SAUTU YA DAVID SHEARER )

“Vitendo hivi ni ukiukwaji dhahiri wa sheria za kimataifa za ibinadamu za za haki za binadamu, tunahitaji kuwatafuta wahusika na kuwafikisha mbele ya mkono wa sharia.”

Kwa mujibu wa UNMISS kupelekwa kwa walinda amani hao Unity kutasaidia kufanyika kwa doria hasa katika maeneo ya vijijini ambako mauaji na ukatili mwingine mbaya zaidi vinafanyika ili kuwalinda raia na kuzuia kuendelea kwa mapigano, pia itasaidia kuongeza uwepo wa UNMISS katika kituo chao cha Leer ambako raia wengi wanasaka hifadhi.