Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nina hofu na kinachoendelea Gaza- Guterres

Katibu Mkuu wa UM Antonio Guterres
PICHA/UN/Evan Schneider(maktaba)
Katibu Mkuu wa UM Antonio Guterres

Nina hofu na kinachoendelea Gaza- Guterres

Amani na Usalama

Austria, Gaza, DPRK ni miongoni mwa mada alizojadili Katibu Mkuu wa UN akizungumza na wana habari huko Vienna.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres aliyeko ziarani Austria amezungumzia mambo muhimu yanayokumba dunia hivi sasa ikiwemo silaha za nyuklia na ghasia huko ukanda wa Gaza.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mazungumzo na Kansela wa Austria Sebastian Kurz mjini Vienna, Bwana Guterres amesema ingawa kuna tishio la kuendeleza silaha za nyuklia na zile za kemikali..

(Sauti ya Antonio Guterres)

“Wakati mwingine kuna habari n jema na ningependa kutaja moja ambayo inahusiana na tangazo la hivi karibuni la Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK kuwa ina nia ya kufunga eneo la majaribio ya nyuklia huko Punggye-ri. Napenda kukaribisha na kusema kufunga kabisa eneo hilo itakuwa muhimu katika kujenga Imani na kuchangia katika juhudi za amani endelevu na ukaguzi wa kuthibitika wa kuondoa nyuklia rasi ya Korea.”

Na kuhusu ghasia zinazoendelea huko Ukanda wa Gaza baada ya Marekani kuhamishia rasmi hii leo ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda mji wa Yerusalem, Bwana Guterres amesema..

(Sauti ya Antonio Guterres)

“Nina hofu kubwa leo kutokana na ripoti kuhusu kinachoendelea Gaza, tayari idadi kubwa ya watu wameuawa.”

Kuhusu Austria ambayo kesho inaadhimisha miaka 63 tangu ipate uhuru na mamlaka kamili, Katibu Mkuu amesifu uhusiano bora kati ya Umoja wa Mataifa na taifa hilo hususan mchango wake katika kumairisha amani na usalama duniani.

TAGS: Antonio Guterres, Austria, Gaza, DPRK