Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakunga ni chachu ya huduma bora kwa mama na mtoto: WHO

Mkunga Helen Danies anazungumza na mama mgeni katika wodi ya kinamama hospitalini Juba, Sudan Kusini Jumatatu Januari 2018
UNICEF/UN0159224/Naftalin
Mkunga Helen Danies anazungumza na mama mgeni katika wodi ya kinamama hospitalini Juba, Sudan Kusini Jumatatu Januari 2018

Wakunga ni chachu ya huduma bora kwa mama na mtoto: WHO

Wanawake

Kila sauti hiyo isikikapo wakati mama anajifungua huwa ni muziki masikioni mwake, lakini mamilioni ya watoto na kina mama duniani hupoteza maisha kila mwaka sababu ya kukosa dumuma bora wakati wa ujauzito, kipindi cha kujifungua na hata baada ya kujifungua, kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO.

(Picha:UNNewsKiswahili/Assumpta Massoi)
Akupokeaye nawe mtunze

Shirika hilo linasema wanawake na watoto wachanga kote duniani wana haki ya kupata huduma bora na itakayowawezesha kuwa na uzuoefu mzuri wakati wa kujifungua na hata baada ya hapo ambayo inajumuisha heshima, utu, kuwa na chaguo, mawasiliano bayana kutoka kwa wauguzi wanaohusika na masuala ya uzazi, mikakati bora ya kupunguza maumivu, uwezo wa kina mama kufika kliniki na maamuzi ya njia ya kujifungua.

Hilo linawezekana tu kwa msaada mkubwa wa wakunga wenye uzoefu na ujuzi unaostahil limesema shirika la WHO katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya wakunga duniani ambayo kila mwaka huwa Mei 5. Na limetoa muongozo kuhusu umuhimu wa wakunga kwa mustakhbali wa mama na mtoto. Elizabeth Iro afisa mkuu wa wauguzi wa WHO anaeleza kwa nini

(SAUTI YA ELIZABETH IRO)

“Kwanza ni kuhusu utoaji wa huduma na kuhusu ushahidi wa jinsi ya kuhakikisha uzoefu mzuri wa kujifungua kwa wanawake, pili na ni kwa mara ya kwanza, muongozo huo unapendekeza   wakunga kushika usukani wa humuma endelevu, na inaonyesha kwamba sio tu ni huduma hiyo endelevu ndiyo inayopendwa na wanawake lakini pia inafaida kubwa ikiwemo kupunguza kwa asilimia 24 kujifungua kabla ya wakati.”

Image
Mkunga Christy Anya. Picha:Video Capture/World Bank

Kauli mbiu ya siku ya wakunga mwaka huu ni “wakunga wanaongoza kwa huduma bora”. WHO inasema ushahidi unaonyesha kwamba  wakunga walioelimika na kufuzu kufikia viwango vya kimataifa wanaweza kutoa asilimia 87 ya huduma inayohitajika na kina mama na watoto wachanga, pia wanawake wanaopata huduma ya muendelezo ya wakunga ainayopendekewa na WHO,  hupunguza kwa asilimia 24 uzazi wa kabla ya wakati, asilimia 16 hatari ya kupoteza watoto na hueleza kuridhika na mazingira ya kujifungua kwa kiasi kikubwa.

Shirika hilo linasisitiza ni lazima kuhakikisha kwamba wanawake wote wanapata fursa ya huduma endelevu inayotolewa na wakunga walioelimika na kufuzu na wanaosimamia na viwango vya kimataifa vya wakunga.