Bloomberg atoa dola milioni 4.5 kupambana na mabadiliko ya Tabianchi-UN

22 Aprili 2018

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa, kuhusu mabadiliko ya tabianchi,Michael Bloomberg, ametangaza kutoa dau la  dola milioni 4.5 kwenda kwa fuko la  Umoja wa Mataifa linalohusika na  nabadiliko ya tabianchi UNFCCC.

Pesa hizo ni zitasaidia UNFCC kutekeleza majukumu yake kwendana na mkataba wa Paris.
Tajiri huyu muhisani na meya wa zamani wa jiji la New York, Juni mwaka jana aliahidi kujaza pengo la fedha la idara hiyo lililosababishwa na  hatua ya rais wa Marekani, Donald Trump, kutangaza kujiondoa kutoka kwenye  mkataba wa Paris kuhusu tabianchi wa mwaka 2015.

Mchango wa Bloomberg utasaidia katika operesheni za ujumla kama vile kusaidia nchi kufikia malengo yake  ya kupunguza gesi za viwandani kwendana na makubaliano yaliyofikiwa na mataifa 193 katika mji mkuu wa Paris nchini Ufaransa.
 
Taarifa iliyotolewa na idara ya habari ya Bloomberg, inanukuu baraza ka Congress la Marekani likitangaza kupunguza mgao wa mwaka huu kwa idara ya UNFCCC kwa kiasi cha dola milioni nne unusu yaani kutoka dola milioni saba unusu hadi dola  milioni tatu.
Akitangaza mchango wake kupitia kipindi cha Televisheni ya CBS cha ‘Face the Nation”, bwana Bloomberg amesema kuwa Marekani ilitoa ahadi na yeyé kama  Mmarekani, nawajibika ,ikiwa serikali haitatekeleza ahadi yake kutekeleza wajibu huo.

Nae Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter, amemsifu Michael Bloomberg sio tu kwa uhisani wake kwa Umoja wa Mataifa lakini pia kuwa mstari wa mbele kuhusu msuala ya mabadiliko ya tabianchi duniani.
Shirika la UNFCCC linasema mchango huu umekuja kwa wakati muafaka na  Katibu Mtendaji wake, Patricia Espinosa, amesema kuwa, mchango huu anaukaribisha kwa mikono miwili kwani ni msaada unaodhirisha  haja ya kushirikiana kutekeleza wajibu wetu kuhusu tabianchi.

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter