Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghana yatakiwa kuziba pengo la kiuchumi ili kufikia SDGs 2030

Wachuuzi wauza bidhaa zao katikati ya magari katika trafiki huko Tema, Ghana. Picha: Jonathan Ernst / World Bank (maktaba)

Ghana yatakiwa kuziba pengo la kiuchumi ili kufikia SDGs 2030

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Mtaalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na kutokomeza umasikini ametoa wito kwa serikali ya Ghana kutoa kipaumbele katika haki za kijamii hususani suala matabaka kati ya matajiri na masikini ili kufikia melengo ya maendeleo andelevu  SDG’s ifikapo mwaka 2030.

Akimaliza ziara yake ya siku 10 jijini Accra na miji mingine ya kaskazini mwa nchi hiyo, Bw Philip Alston amesema , Ghana nchi inayojulikana kama kinara wa demokrasia barani Afrika ina jukumu la kuchagua kati ya mfumo wa kiuchumi wa sasa ambao unawatajirisha waliokuwa nacho au kuingia katika mfumo utakao wajumuisha watu wote ikiwemo mamilioni ya masikni nchini humo.

 Ameongeza kuwa ripoti za kiuchumi kati ya mwaka 2012-2013 zinaonyesha kuwa robo ya raia wa nchini hiyo wanaishi katika umasikini na mtu mmoja kati ya 12 anaishi katika ufukara huku wanasiasa na walio madarakani wakiishi maisha ya kifahari.

Amesema changamoto hivi sasa ni kwa aserikali kuchagua vipaumbele vyake na kuhakikisha hifadhi ya jamii ni miongoni mwa vipaumbele hivyo.

Ripoti hiyo kuhusu matabaka ya kiuchumi nchini Ghana itawasilishwa mwezi Juni katika kikao kijacho cha baraza la haki za binadamu  la  Umoja wa Mataifa jijini Geneva Uswis .