Kuna pengo kubwa la usawa baina ya nchi na nchi:UN ripoti

11 Julai 2019

Kuna pengo kubwa la  usawa kati ya nchi moja na nyingine, na miongoni mwa maeneo maskini katika jamii kwa mujibu wa ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa liyotolewa leo Alhamisi.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP, vipimo vya umaskini kimataifa mwaka huu wa 2019 vinaonyesha kwamba katika nchi 101 ambako kumefanyika utafiti, nchi 31 za kipato cha chini, 68 za kipato cha wastani na mbili za kipato cha juu watu bilioni 1.3 ni maskini wa kila hali yaani  sio tu kipato lakini pia, kiafya, ubora wa kazi na hatari ya ukatili.

Umaskini uko kila mahali, ukosefu wa usawa ndani ya nchi ni mkubwa

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya UNDP, hatua zinahitajika katika nchi zote zinazoendelea imesema ripoti na kwamba kusini mwa jangwa la Sahara na Asia Kusini kuna idadi kubwa zaidi ya watu maskini ikiwa ni asilimia 84.5.

Ripoti imetaja viwango vya ukosefu wa usawa katika kanda kama vya juu; ambako Kusini mwa jangwa la Sahara viwango ni asilimia 6.3 Afrika Kusini na 91.9 nchini Sudan Kusini. Tofauti ya viwango vya umaskini Asia Kusini ni kutoka asilimia 0.8 huko Maldives hadi 55.9 nchini Afghanistan.

Nyingi ya nchi ambazo zimefuatiliwa katika ripoti zinaonyesha kwamba kuna ukosefu wa usawa mkubwa ndani ya nchi binafsi kwa mfano nchini Uganda, umaskini wa aina nyingi katika jimbo tofauti ni kati ya asilimia 6 mjini Kampala hadi asilimia 96.3 Karamoja.

Watoto wanabebe mzigo mkubwa

Zaidi ya nusu ya watu bilioni 1.3 wanaotajwa kama maskini, watu milioni 663 ni watoto wa chini ya umri wa miaka 18 na takriban theluthi moja sawa na watu milioni 428 ni watoto wa chini ya umri wa miaka kumi.

Ripoti imesema wengi wa watoto hawa, takriban asilimia 85 wanaishi Asia Kusini na kusini mwa jangwa la Sahara idadi ikiwa karibia nusu katika kila ukanda. UNDP imsema taswira ni mbaya Zaidi nchini Burkina Faso, Chad, Ethiopia, Niger na Sudan Kusini ambako asilimia 90 au zaidi ya watoto walio na chini ya umri wa miaka 10 wanatajwa kuwa maskini wa kila hali.

Ishara ya hatua kufikia kupunguza umaskini

Ripoti imetathmini hatua zilizopigwa katika kufikia lengo la kwanza la malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu ikiwemo ni kupunguza umaskini katik mifumo yote duniani kote.

Ripoti imetambua nchi kumi ambazo kwa apmoja zina idadi ya watu takriban bilioni 2 na kwa ajili ya kuonyesha viwango vya kupunguza umaskini na zote zimeonyesha kwamba kwa mujibu wa takwmiu, hatua kubwa zimepigwa kuelekea kufikia lengo la kwanza. Huku kupungua kwa viwango kwa kasi vimeshuhudiwa nchini India, Cambodia na Bangladesh.

Hatahivyo ripoti imeonya kwamba hakuna kipimo kimoja ni muongozo hakika wa kuonyesha taswira ya ukosefu wa usawa na umaskini wa hali zore na kwamba tafiti kama ya viwango vya maendeleo ya binadamu na Ilie ya kupima usambazaji wa kipato nchini zinaweza kutoa tarifa muhimu kwa ajili ya será za kupunguza umaskini kikamilifu.

 

 

  

 

 

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud