Tumechukua hatua kurahisisha maisha ya wakazi wa mijini- Kenya

13 Aprili 2018

Mkutano wa 51 wa kamisheni ya idadi ya watu ya Umoja wa Mataifa ukikunja jamvi hii leo jijini New York, Marekani, serikali ya Kenya imejinasibu hatua ambazo imechukua kuhakikisha kuna miji endelevu inayorahisisha maisha ya wakazi wa mijini.

Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kando ya mkutano huo, Nzomo Mulatya ambaye ni Naibu Mkurugenzi wa Baraza la Kitaifa la idadi ya watu nchini Kenya ametaja hatua hizo kuwa ni pamoja na ujenzi wa reli kubwa ya kisasa, au Standard Gauge Railway akisema..

(Sauti ya Nzomo Mulatya)

Maudhui ya mkutano yalilenga pia miji jumuishi, endelevu na masuala ya uhamiaji ambapo Bwana Nzomo amezungumzia kile watakachoendelea nacho wakirejea nyumbani Kenya.

(Sauti ya Nzomo Mulatya)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter