Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi wa Afrika Mashariki waendelea kukua- ECA

Mbele ya Duka nchini Kenya, ukuaji wa biashara halisi umeimarisha uchumi nchini humo..Picha: ILO

Uchumi wa Afrika Mashariki waendelea kukua- ECA

Ukuaji wa Kiuchumi

Kipato cha wastani katika ukanda wa Afrika Mashariki kimeongezeka maradufu katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, kikifikia kiasi cha dola za Marekani 740 kwa mtu mwaka 2016. 

Taarifa hizo ni kwa mujibu wa ripoti ya mpya kuhusu maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika ukanda huo iliyozinduliwa leo huko Kigalin chini Rwanda.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Uchumi wa Afrika, ECA, ofisi ya Afrika Mashariki, Andrew Mold amesema uchumi wa Afrika Mashariki umekua kwa kiasi cha takriban asilimia 6.5 kati ya mwaka 2012 na 2016, kiwango cha juu zaidi kuliko sehemu zingine zote duniani wakati huo.

Kwa mwaka 2018, wachumi wanategemea kuwa ukuaji wa uchumi utafikia asilimia 5.9, ukinufaika zaidi na uwekezaji mkubwa katika miundombinu.

Naye Balozi wa Kenya nchini Rwanda, John Mwangemi, amesema ushirikiano zaidi unahitajika katika kutekeleza mipango ya maendeleo ya viwanda, akitoa mfano wa utengenezaji wa magari.

Amesema Kenya inaunga mkono mkataba wa eneo huru la biashara  Afrika, CFTA akisema..

(Sauti ya Balozi John Mwangemi)