Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Eneo la biashara huru Afrika kumkomboa mfanyabiashara mwanamke

Katibu Mtendaji wa tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika, ECA, Vera Songwe akihutubia kikao cha Baraza tendaji la Muungano wa Afrika, AU mjini Kigali nchini Rwanda hii leo
ECA/Priscilla Lecomte
Katibu Mtendaji wa tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika, ECA, Vera Songwe akihutubia kikao cha Baraza tendaji la Muungano wa Afrika, AU mjini Kigali nchini Rwanda hii leo

Eneo la biashara huru Afrika kumkomboa mfanyabiashara mwanamke

Wanawake

Eneo la biashara huru barani Afrika litaimarisha biashara hususan zinazofanywa na wanawake kwa kuvuka mipaka kutoka nchi moja hadi nyingine. 

Katibu Mtendaji wa tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika, ECA, Vera Songwe, amesema hayo hii leo huko Kigali Rwanda, wakati akifungua kikao cha kamati tendaji ya Muungano wa Afrika, AU.

Amesema zaidi ya theluthi mbili ya wafanyabiashara wasio rasmi mipakani ni wanawake ambao hukumbwa na manyanyaso na ukatili.

(Sauti ya Vera Songwe)

“Makubaliano ya biashara huru Afrika yatarahisisha mfumo wa biashara ya mipakani na kuweka mazingira bora kwa wafanyabiashara Afrika.  Yataimarisha pia matumizi ya rasilimali kwa sababu kadri tunavyofanya biashara baina yetu, tunahakikisha mapato yetu yanaongezeka kadri tunavyowabadili wafanyabiashara wanawake ili wawe sekta rasmi binafsi inayochangia mapato ya serikali na pia kunufaika na mifumo iliyowekwa kuhakikisha biashara ni huru na ya uhakika.”

Image
UN Photo/Evan Schneider
Wanawake wajasiriamali nchini Tanzania. Picha:

Halikadhalika Bi.  Songwe amezungumzia vijana akisema kuwa makubaliano ya biashara huru Afrika yatapanua wigo wa aina ya biashara na hivyo kutoa fursa kwa vijana badala ya kutegemea bidhaa za mitaji mikubwa kwenye uzalishaji kama vile petrol na madini.

Makubaliano hayo yanamaanisha kuwa wafanyabiashara na walaji hawatalipa ushuru kwa aina nyingi za bidhaa zinazouzwa baina ya nchi za Afrika na yatatiwa yatatiwa saini tarehe 21 mwezi huu huko Kigali.