Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICT ni chachu ya kumuwezesha mwanamke wa kijijini: FAO/IFAD/WFP

iHub ni kituo cha ubunifu na biashara kupitia teknolojia nchini Kenya.
Picha: iHub/UNDP
iHub ni kituo cha ubunifu na biashara kupitia teknolojia nchini Kenya.

ICT ni chachu ya kumuwezesha mwanamke wa kijijini: FAO/IFAD/WFP

Wanawake

Teknolojia ya Habari na mawasiliano ICT imeelezwa kuwa ni muhimu sana katika kumkomboa mwanamke wa kijijini.

Hayo yameelezwa leo kwenye mjadala wa siku ya wanawake duniani ulioandaliwa na shirika la kimataifa la ufadhili wa maendeleo ya kilimo IFAD mjini Roama Italia.

Mjadala huo uliohusisha mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa ikiwemo la kilimo na chakula FAO na la mpango wa chakula duniani WFP  na kuwasilisha ripoti mpya ya usawa wa kijinsia na matumizi ya ICT kwa kilimo na maendeleo vijijini , ulijikita katika jukumu la teknolojia ya Habari na mawasiliano katika kusaidia wanawake wa kijijini kuwezeshwa kiuchumi, kuwapa sauti na hadhi.

Mashirika hayo yamesema upanuzi wa wigo wa ICT kwa wanawake wa vijijini utawapa fursa za kushiriki katika masoko, kupata elimu na taarifa muhimu kwao.

Kwa mujibu wa utafiti wa mashirika hayo wanawake wkipata fedha mara nyingi tofauti na wanaume watazitumia fedha hizo katika kununua chakula cha familia zao na kusomesha watoto wao.

Kostas Stamoulis ni mkurugenzi msaidizi wa idara ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii wa FAO.

(SAUTI YA KOSTAS STAMOULIS)

“Kwa bahati mbaya licha ya uwezo wa ICT kuwawezesha wanawake, wanawake wa vijijini katika nchi zinazoendelea wanakabiliwa na changamoto tatu, mosi wanaishi katika nchi zinazoendelea ambako kuna pengo kubwa la upatikanaji wa ICT’s pili wanaishi vijijini ambako kuko nyuma zaidi na tatu kwa sababu ni wanawake hivyo fursa yao ya ICT iko nyuma sana”