Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake washirikishwe katika utatuzi wa migogoro: Zerrougui

Leila Zerrougui,Mkuu wa kikosi cha Umoja wa Maaifa cha kulindfa amani jamhuri ya Kidemokrasis ya Kongo-MONUSCO akiongea.
Picha ya UN /Manuel Elias
Leila Zerrougui,Mkuu wa kikosi cha Umoja wa Maaifa cha kulindfa amani jamhuri ya Kidemokrasis ya Kongo-MONUSCO akiongea.

Wanawake washirikishwe katika utatuzi wa migogoro: Zerrougui

Wanawake

Wakati umefika kuwawezesha  wanawake kuhusika katika shughuli za kutatua migogoro mbalimbali.

Hayo yametamkwa na Bi Leila Zerrougui, mkuu wa kikosi cha MONUSCO, kikosi ambacho ni cha Umoja wa Mataifa kinacholinda amani Congo katika mazungumzo yake na  UNNews wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Ametoa kauli yake kuhusu mchango wa mwanamake ,  katika ngazi za uongozi.

(SAUTI YA LEILA)

Nadhani ni muhimu kuwa na viongozi wanawake katika muktadha kama huu kwa sababu, kwa muda mrefu una wanaume ambao wanajihusisha na migogoro ambayo waathirika wake wakubwa ni wanawake na watoto. Kwa hivyo nadhani mwelekeo wa mwanamke  ambae ana uelewa wa kutosha pamoja na ujuzi ni muhimu mno kwa sababu utapata taswira tofauti ya wanaume na wnawake

Amesema kuwa mseto wa mwanamme na mwanamke utaleta msukumo wa jinsi ya kuangalia masuala kwa mitazamo tofauti  vile kutilia mkazo waathirika, na kile kinachoweza kupatikana sio tu kupitia mapigano au vita lakini kuwaelewesha wananchi ambao wako katika taifa linalopitia migogoro ya ndani kuwa, ufumbuzi  sio tu kupitia  mabavu lakini pia kupitia njia za  amani.