Warohingya wanastahili kuona hali halisi kabla ya kurejeshwa Mnaymar:Grandi
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi , UNHCR linaunga mkono mchakato endelevu wa kuwarejesha nyumbani kwa hiyari wakimbizi wa Rohingya au watakapochagua endapo zoezi hilo lizingatia misngi ya haki za binadamu , usalama na utu na litashirikiana na wadau wote kutimiza azma hii.
Kauli hiyo imetolewa leo na Kamishina mkuu wa wakimbizi Filipo Grandi akisistiza kuwa kurejeshwa huko lazima kuzingatie matakwa ya wakimbizi hao, wawe wamepewa taarifa za kutosha kabla ya kufanya maamuzi , na kutathimini mbikimbizi mmojammoja kabla ya kurejeshwa.
Ameongeza kuwa ni muhimu kuhakikisha kuwa kurejea huko kunafanyika tu endapo ni hiyari yao kutokana na uelewa sahihi walionao wa mazingira yaliyopo nchini mwao na mahali watakapkorejea.
Grandi amesema njia nzuri ya kuwahakikishia ufahamu huo wakimbizi wa Rohingya walioko Bangladesh ni kuwaruhusu kwenda kujionea wenyewe hali halisi nchini Myanmar.
Kabla ya kuamua endapo watarejea ama la wakimbizi hao walioarifiwa kuhakikiwa na serikali ya Myanmar kwamba wana haki ya kurejea nyumbani , UNHCR inataka waruhusiwe kutembelea maeneo walikotoka kwenye jimbo la Rakhine, au maeneo mengine watakayochagua kurejea ili waweze kufanya tathimini ya endapo wanahisi wataweza kurejea mahali hapo kwa usalama na utu.
Grandi amesisitiza kuwa “Uongozi wa Myanmar ni lazima uwaruhusu wakimbizi hawa kufanya hivyo bila masharti na kukiuka haki zao za kurejea nyumbani katika siku za usoni , na endapo baada ya kuzuru maeneo hayo wakimbizi wataamu mazingira hayawaruhusu kurudi jimbo la Rikhine kwa utu na usalama.”
UNHCR inasema wajibu wa kuboresha mazingira hayo uko mikononi mwa Myanmar ingawa shirika hilo haliamini kwamba mazingira ya sasa Rakhine yanaridhisha kwa wakimbizi hao kurejea kutoka Bangladesh kwa hiyari, usalama , utu na endelevu.
Lakini linasema litaendelea na ahadi yake ya kusaidia juhudi za serikali ya Myanmar za kuweka mazingira bora chini ya makubaliano yaliyotiwa saini na UNHCR, shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, na uongozi wa Myanmar mwezi June .
Kamishina Mkuu wa wakimbizi amesema “Tunaendelea kuishukuru serikali ya Bangladesh ikiendelea na ukarimu wake wa kuwahifadhi wakimbizi wa Rohingya hadi pale watakapoweza kurejea kwa hiyari, utu na usalama nchini Myanmar.”