Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kilimo cha kisasa dawa mujarabu ya mabadiliko ya tabia nchi

Fatoou Yalindiaye kutoka Senegal. Picha: UM/Video capture

Kilimo cha kisasa dawa mujarabu ya mabadiliko ya tabia nchi

Ajenda ya maendeleo endelevu ya  mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa  inahimiza nchi zote wanachama kuwekeza katika kilimo cha kisasa ili kukabiliana na changamoto za mbadiliko ya tabia nchi na pia uhabibifu wa mazingira.

Nchini Senegal Afrika magharibu serikali kwa kushirikana na mashirika ya kibinadamu wameitikia wito huo ili kusaidia wananchi katika kutoa elimu ya kilimo cha kisasa katika kupambana na matatizo ya ukame unaokumba nchi nyingi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la sahara.

katika makala yetu ya leo Siraji Kalyango wa Idhaa ya kiswahili anatupeleka katika kijiji cha Louga nchini Senegal ambako mmoja wa wakulima mama Fatou anaeleza mbinu wanazotumia kukabiliana na ukame