Ushelisheli yajizatiti kulinda msingi wake wa uchumi

18 Disemba 2017

Umoja wa  Mataifa  na washirika wake wamekuwa mstari wa mbele katika suala la mazingira kama ilivyo katika lengo namba 13  la ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 kuhusu mazingira na tabianchi. Katika mkutano wa Paris wa mwaka 2015, nchi wanachama walipitisha mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi wenye lengo la kudhibiti shughuli za kiuchumi au kijamii zinazozalisha hewa ya ukaa, huku wakipigia chepuo utunzaji wa mazingira.Katika kutekeleza hilo nchi wanachama zinafanya kampeni za utunzaji bahari na viumbe wa baharini na leo tunaelekea  katika visiwa vya Ushelisheli ambako Patrick Newman anakuletea makala  kuhusu jitihada za serikali ya visiwa hivyo za kutunza bahari ambayo ni tegemeo kubwa kwa  uchumi wan chi hiyo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud