Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lengo la usawa wa kijinsia liende sambamba na kutokomeza umaskini- TAMWA

Balozi wa Canada nchini Tanzania Ian Myles(kulia) akiteta jambo na viongozi wa TAMWA, kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa TAMWA Alakok Mayombo, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Edda Sanga na Meneja wa Mipango wa TAMWA Devis Lumala. (PICHA: Kwa hisani ya TAMWA)

Lengo la usawa wa kijinsia liende sambamba na kutokomeza umaskini- TAMWA

Wakati chama cha waandishi wa habari wanawake nchini Tanzania, TAMWA hii leo kikitimiza miaka 30 tangu kuundwa chake, chama hicho kimesema malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs, yamekuwa ni kichocheo katika kumkwamua mwanamke.

Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga ameiambia Idhaa hii kuwa lengo namba tano kuhusu usawa wa kijinsia lilionekana kama ni zawadi katika kumkwamua mwanamke lakini hata hivyo…

(Sauti ya Edda Sanga)

Bi.  Sanga akaelezea vile ambavyo wamekuwa mstari wa mbele si tu kuwezesha wanawake wengine bali pia wanachama wa TAMWA ili waweze kufanya kazi yao kwa ufanisi katika  jamii.

image
Miongoni mwa mijadala wakati wa kuelekea maadhimisho ya miaka 30 ya TAMWA. (Picha:Kwa hisani ya TAMWA)
(Sauti ya Edda Sanga)

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TAMWA akatoa wito kwa waandishi wa habari wa Kike na wa kiume akitaka wazingatie ueledi na misingi ya tasnia hiyo ikiwemo utafiti kama njia mojawapo ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii.