Mwanamuziki ‘Double D’ wa DRC atumia muziki kukemea ukatili wa kingono

Mwanamuziki ‘Double D’ wa DRC atumia muziki kukemea ukatili wa kingono

Ukatili wa kingono kwenye maeneo ya mizozo ni jambo ambalo Katibu Mkuu wa sasa wa Umoja wa Mataifa António  Guterres ameazimia kukabiliana nalo. Bwana Guterres ameguswa zaidi na vitendo hivyo kwa kuzingatia pia baadhi yao vinatekelezwa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa kwenye maeneo ambako wanalinda amani. Tayari amechukua hatua hata kwa kuteua mtetezi wa wahanga wa vitendo hivyo dhalili. Sasa na makundi mbalimbali yamejitokeza kuunga mkono harakati hizo za kusaka haki zao na pia kuwapa moyo na miongoni mwao ni mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC aitwae Dube David al maaruf Double D. Grace Kaneiya katika makala hiyo anaangazia harakati za Double D za kusongesha harakati za Umoja wa Mataifa.