Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maigizo yasaidia kurejesha utangamano Sierra Leone

@UNICEF

Maigizo yasaidia kurejesha utangamano Sierra Leone

Sierra Leone ni nchi inayoendelea kujijenga upya baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kuanzia mwaka 1991 hadi 2002. Jitihada za kimataifa zinaendelea ili kuhakikisha kunakuwepo utangamano miongoni mwa wananchi. Miongoni mwa juhudi hizo ni zile zinazofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF za kutumia maigizo kutokomeza ghasia na ukatili miongoni mwa wanajamii. Ukatili huo ni pamoja na vipigo vya watoto kama inavyobainisha makala hii inayosimuliwa na Assumpta Massoi.