Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikishaji wananchi DRC wasaidia kupunguza ukatili wa kingono

Ushirikishaji wananchi DRC wasaidia kupunguza ukatili wa kingono

Leo alasiri katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kutafanyika kikao cha ngazi ya juu kuhusu unyanyasaji na ukatili wa kingono, SEA, kwenye mizozo ambapo Umoja wa Mataifa pamoja na mambo mengine unaelezea hatua zinazochukuliwa kukabiliana na vitendo hivyo dhalimu ambako kuna operesheni za ulinzi wa amani.

Miongoni mwa maeneo ambako vitendo hivyo vimeripotiwa kufanywa na walinda amani ni katika jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanatekeleza majukumu yao.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wanaelezea hali ilivyokuwa..

(Voxpops)

Hata hivyo tayari Umoja wa Mataifa umechukua hatua mathalani katika eneo la Masisi lililopo jimbo la Kivu Kaskazini wanawake wamejiunga katika mtandao wao uitwao MUWAMA wakishirikisha wanaume ili kukabili vitendo hivyo ambayo awali vilitishia mustakhbali wa amani kwenye eneo hilo.

Charlotte Muongo ni mwenyekiti wa MUWAMA, mtandao ambao umeanza kampeni za kuhamasisha athari za vitendo hivyo, kampeni ambazo zimewezesha hata mazungumzo na walinda amani na sasa anasema…

(Sauti ya Charlotte)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres tayari amesisitiza kuwa kamwe hatokubali mtu yeyote kutekeleza vitendo hivyo vya ukatili wa kingono na unyanyasi na atumia bendera ya Umoja wa Mataifa kujificha.

Amesisitiza kuwa vitendo hivyo kamwe havitavumiliwa na ameweka mkakati wa kudhibiti na hatimaye kutokomeza vitendo hivyo.