Guterres alaani shambulio huko Finland

19 Agosti 2017

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani shambulizi la kigaidi lililotokea jana Ijumaa kwenye mji wa Turku nchini Finland.

Vyombo vya habari vinaripoti kuwa shambulio hilo lilitokea baada ya kijana mmoja kushambulia watu kwa kisu na kusababisha vifo vya watu 9 na wengine wamejeruhiwa.

Kufuatia tukio hilo, Bwana Guterres kupitia kwa msemaji wake, ametuma salamu za rambirambi kwa serikali na wananchi wa Finland huku akiwatakia ahueni ya haraka majeruhi.

Amesema Umoja wa Mataifa unashikamana na serikali ya Finland katika vita dhidi ya ugaidi na misimamo mikali.

Ripoti zinaeleza kuwa kijana mshukiwa wa tukio hilo anashikiliwa na polisi.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter