Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vyama vya ushirika vyaleta nuru ya umiliki wa makazi Kenya

Vyama vya ushirika vyaleta nuru ya umiliki wa makazi Kenya

Kufikia mwaka 2030, takribani asilimia 60 ya wakazi wa dunia watakuwa wakiishi mijini, na idadi kubwa itakuwa kwenye nchi zinazoendelea kama vile Kenya. Upanuzi huu wa kasi wa miji unatia shinikizo katika huduma za kijamii kama vile makazi na mifumo ya maji safi na maji taka.

Ni katika muktadha huo ambapo vyama vya ushirika nchini Kenya vinajaza pengo linaloachwa na sekta rasmi ya benki ili kuwezesha ufadhili wa ujenzi na umiliki wa nyumba kwa wakazi wa mijini kama vile mji mkuu Nairobi. Katika Makala hii inayoletwa kwako na Grace Kaneiya, Benki ya Dunia imeangalia ni jinsi gani serikali ya Kenya inaweza kuchukua fursa ya ukuaji wa miji ili kufanikisha lengo namba 11 la maendeleo endelevu katika makazi bora.