Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bahari ni jinamizi lakini pia ni daraja la maisha mapya kwa wakimbizi

Bahari ni jinamizi lakini pia ni daraja la maisha mapya kwa wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linasema vita vimesababisha maelfu ya watu kutoka Syria kukimbia makazi yao wakielekea nchi za ulaya, hivyo wengi wao ikiwemo watoto takriban 150 wamepoteza maisha yao katika bahari ya Mediterranea. UNICEF linashirikiana na wadau wake kushughulikia ulinzi wa watoto wahamiaji na wakimbizi.

Katika makala ifuatayo Selina Jerobon anaelezea moja ya kisa cha kusikitisha cha kifo cha mtoto kilichoacha majionzi makubwa. Ungana naye.