ESCAP kujadili uhusiano wa kikanda na SDGs

15 Mei 2017

Wakuu wa nchi na maafisa kadhaa wa ngazi juu kutoka ukanda wa Asia na Pasifiki, wanatarajiwa kukutana mjini Bangkok nchini Thailand kwenye mkutano wa siku tano wa Umoja wa Mataifa wa ukanda huo kujadili namna ushirikiano wa kiuchumi katika ukanda huo unavyoweza kusaidia kutimiza malengo ya maendeleo endelevu SDGs.

Kwa mujibu wa taarifa ya wavuti wa tume ya Umoja wa Mataifa ya kiuchumi na kijami kwa ukanda wa Asia na Pacific ESCAP, mkutano huo wa 73 wenye kauli mbiu ushirikiano wa kikanda kwa nishati endelevu utafanyika Mei 15 hadi 19, ambapo kipengele cha ufunguzi wa maafisa waandamizi ni hii leo.

Marais kadhaa wamthibitisha ushiriki wao katika mkutano huo wakiwamo kutoka Nauru, Palau na visiwa vya Marshall, huku pia mawaziri kutoka ukanda huo wakitarajiwa katika majadiliano ya ngazi ya juu,  mada ikiwa ni usaidizi na kutumia fursa ya kiuchumi ya ukanda wa Asia an Pacific katika kutekeleza ajenda ya 2030.

Taarifa hiyo pia inafafanua kuwa mjadala wa mawaziri mnamo Mei 18 utajikita katika muktadha wa kubadilisha nishati katika eneo hilo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter