Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhaba wa chakula wachochea uhamiaji- WFP

Uhaba wa chakula wachochea uhamiaji- WFP

Ukosefu wa uhakika wa chakula pamoja na njaa ni moja ya sababu za watu kukimbia makazi yao, limesema shirika la mpango wa chakula duniani WFP hii leo.

Katika ripoti yake iitwayo Chanzo cha kuondoa: Uhakika wa chakula, migogoro na uhamiaji wa kimataifa, WFP imebaini kuwa kila ongezeko la asilimia moja la ukosefu wa chakula, linasababisha ongezeko la asilimia mbili ya watu wanaohama makwao.

Halikadhalika ripoti hiyo inataja uhamiaji kama moja ya chanzo cha ukosefu wa uhakika wa chakula kwa kuzingatia gharama na ukosefu utulivu miongoni mwa wale wanaohahama.

Akizungumzia ripoti hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa WFP David Beasley amesema wakati huu ambapo mamilioni ya watu wamekimbia makwao, ni wajibu wa jumuiya ya kimataifa kuangazia janga hilo.

Amesema kwa kuelewa mazingira yanayoshinikiza watu kukimbia makwao, watoa misaada ya kibinadamu na wadau wengine wanaweza kutoa vyema misaada inayohitajika.

Hii ni mara ya kwanza kabisa kunafanyika uchambuzi kama huo unaoonyesha uhusiano kati ya ukosefu wa uhakika wa chakula na uhamiaji