Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres akaribisha kuachiliwa huru Iraq raia 26 wa Qatar

Guterres akaribisha kuachiliwa huru Iraq raia 26 wa Qatar

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekaribisha kuachiliwa huru na kurejea nyumbani raia 26 wa Qatar waliokuwa wametekwa kwenye jimbo la Muthanna, nchini Iraq, Desemba 2015.

Kupitia taarifa ya msemaji wake Stephane Dujarric, Katibu mkuu amesea anaelewa kwamba raia hao wa Qatar waliachiliwa bila kudhuriwa, na kuongeza kwamba Umoja wa Mataifa unaishukuru serikali ya Iraq na kwa wote waliochangia kuachiliwa salama mateka hao.