Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Udhalilishaji wa kingono kwenye usafiri wa umma Mexico wakabiliwa

Udhalilishaji wa kingono kwenye usafiri wa umma Mexico wakabiliwa

Kampeni mpya ya kukabiliana na udhalilishaji wa kingono kwenye mfumo wa usafiri wa umma mjini Mexico City . Utafiti wa karibuni uliofanywa nchi nzima emebaini kwamba karibu asilimia 90 ya wanawake wanahisi kutokuwa salama kusafiri kwa mabasi na tren za chini ya ardhi.

Kufuatia takwimu gizo kitengo cha Umoja wa Mataifa cha masuala ya wanawake UN women kwa ushirika na serikali Mexico city wamezindua kampeni kukabiliana na hali hiyo. Yeliz Osman, ni mratibu wa UN Women kuhusu usalama wa miji na maeneo ya umma nchini Mexico

(Sauti ya Yeliz)

“Aina ya udhalilishaji wa kingono tunaojaribu kukabiliana nao katika kampeni hii ni uliofanywa kuwa mazoea na kuhalalishwa katika jamii na wanaume hata hawatambui kwamba huo ni moja ya aina za ukatili na hawajui athari zake kwa wanawake na wasichana na lengo la kampeni ni kuelimisha athari za udhalilishaji huo kwa wanawake na wasicha na tukitumai tutaleta mabadiliko.”