Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kusambaratika kwa mfumo wa afya Yemen kwatishia uhai wa wajawazito- UNFPA

Kusambaratika kwa mfumo wa afya Yemen kwatishia uhai wa wajawazito- UNFPA

Miaka miwili ya mapigano nchini Yemen, imekuwa mzigo mkubwa kwa afya ya wanawake na wasichana nchini humo.

Makala iliyochapishwa katika tovuti ya shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA inasema kuwa mapigano hayo ya wenyewe kwa wenyewe yaliyoanza tarehe 26 mwezi Machi mwaka 2015, yamesambaratisha vituo vya afya, na sasa wanawake wajawazito 52,800 wako hatarini kupata matatizo ya kiafya yanayoweza kusababisha kifo wakati wa kujifungua.

UNFPA imemnukuu mkunga mmoja kwenye jimbo la Lahj anayefanya kazi kwa usaidizi wa shirika hilo akisema kuwa siku moja ya mapigano makali aliitwa kumsadia mwanamke mmoja aliyejifungua nyumbani bila usaidizi wowote kwa kuwa alikuwa hatarini kufariki dunia.

Kwa mantiki hiyo shirika hilo sasa linashirikianana wadau kuimarisha afya ya uzazi kwa wanawake na watoto pamoja na kuwapatia vifaa vya kujisafi wakati wa hedhi.

Mwaka jana pekee, UNFPA ilisambaza nchini Yemen vikasha 80,000 vya kujisafi vikilenga wanawake na wasichana zaidi ya 130,000 pamoja na kuweka vifaa vya kusaidia watoto waliozaliwa njiti