Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rambirambi zaendelea kutolewa kufuatia kifo cha Vitaly Churkin

Rambirambi zaendelea kutolewa kufuatia kifo cha Vitaly Churkin

Salamu za rambirambi kwa mwanadiplomasia mkongwe wa Urusi kwenye umoja wa Mataifa kutoka Vitaly Churkin, zimeendelea kumiminika kufuatia kifo chake cha ghafla Jumatatu , siku moja kabla ya kutimiza miaka 65 ya kuzaliwa.

Katika taarifa yake Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa António Guterres , amemuelezea Churkin mwanadipliomasia mwenye heshma kubwa na uwepo wa haja kwa zaidi ya muongo kwenye baraza la usalama.

Katika upande mwingine wa bahari ya Atlantic mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa Geneva Michael Moller pia ameomboleza kifo cha nguli huyo ambaye ameitumikia serikali ya shirikisho ya Urusi kwa zaidi ya miaka 40.

Akihutubia mkutano wa upokonyaji silaha hii leo Bwana Moller ametoa ujumbe binafsi wa rambirambi kwa familia na jumuiya ya kimataifa kabla ya kumuita balozi Churkin kuwa ni “jabali miongoni mwa wanadiplomasia na atakumbukwa daima”.