Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Balozi wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa afariki dunia

Balozi wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa afariki dunia

Balozi wa kudumu wa Urusi kwenye Umoja wa mataifa Vitaly Churkin amefariki dunia ghafla mjini New York Marekani. Leo baraza kuu la Umoja wa Mataifa limekaa kimya kwa dakika moja wakati wa kikao chake ili kumkumbuka balozi huyo. Balozi wa emarati kwenye Umoja wa Mataifa Lana NNusseibeh ndiye aliyetangaza msiba huo.

(SAUTI YA LANA NNUSSEIBEH)

Wafanyakazi wenzangu, waheshimiwa kwa masikitiko makubwa nawaarifu kwamba ujumbe wa Urusi umetufahamisha kufariki kwa ghabla kwa balozi Vitaly Churkin asubuhi ya leo, kwa niaba yetu sote napenda kutoa salamu za rambirambi , kwa nchi na serikali ya Urusi, kwa ubalozi wa Urusi hapa kwenye Umoja wa Mataifa na zaidi ya yote kwa mke na watoto wawili wa balozi Vitaly Churkin , alikuwa ni mfanyakazi mweznetu, na mwanadfiplomasia aliyejitoa kwa taifa lake na mmoja wa watu wazuri tuliowahi kuwafahamu. Na katika kumkumbuka ningependa tukae kimya kwa muda tafadhali simameni”

Na baada ya dakika moja ya ukimya akizungumzia msiba huo mkubwa kwa Urusi naibu balozi wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa Petr Llyich amesema pengo aliloliacha kwa nchi yake halizibiki na kwamba

(SAUTI YA PETER LLYICH- MSAMI)

“Balozi Churkin amefanya kazi hadi dakika ya mwisho , alitoa maisha yake yote kutetea maslahi ya Urusi , akiwa msitari wa mbele katika diplomasia hasa katika wakati mgumu . Tumepoteza mwanadiplomasia shupavu, mpatanishi imara, mtu mzuri na mwalimu. Hivyo ndivyo tutakavyomkumbuka,. Tunashukuru kwa mshikamano wenu , huruma yenu na msaada wenu katika wakati huu mgumu.”

Churkin amekuwa balozi wa Urusi kwenye Umoja wa mataifa tangu April 2006, kabla ya hapo alikuwa akiwakilisha kibalozi taifa lake nchini Canada na Ubelgigi. Jumanne ya Fenruari 21 Chrkin angekuwa anasherehekea miaka 65 ya kuzaliwa.