Skip to main content

Tamasha la filamu za usalama barabarani laanza leo-UNECE

Tamasha la filamu za usalama barabarani laanza leo-UNECE

Tamasha la kimataifa la siku mbili la filamu za usalama barababarani limeanza leo Jumatatu mjini Geneva Uswis. Kwa mujibu wa kamati ya Umoja wa mataifa ya uchumi kwa mataifa ya Ulaya UNECE ambayo ni mtayarishaji wa tamasha hilo, linafanyika sanjari na maadhimisho ya miaka 70 ya tume ya usafiri wan chi kavu ITC.

UNECE inasema filamu inaweza kuwa nyenzo muhimu sana katika kufikisha ujumbe , hivyo filamu kuhusu usalama barabarani zitasaidia katika kuelimisha umma kuhusu hatari barabarani, zitasaidia kupunguza hatari hizo, kwa kujenga utamaduni wa kuwa na hulka ya kuheshimu sheria, kujenga miundombinu bora na kuruhusu kutumia magari na vifaa salama.

Tamasha hilo litahusisha washiriki wa ngazi ya juu wa mkutano wa mwaka 2017 wa ITC ambao wengi ni wafanya maamuzi kuhusu sera za usalama barabarani na utekelezaji wake.

Pia lengo linguine kubwa la tamasha hilo ni kuwafanya watayarishaji wa filamu kushiriki kinyang’anyiro cha fililamu bora ya usalama barababarani 2017 na tuzo zingine mbalimbali.