Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kazi zenye hadhi kwa ajili ya haki za kijamii-ILO

Kazi zenye hadhi kwa ajili ya haki za kijamii-ILO

Katika kuadhimisha siku ya haki za kijamii duniani Februari 20 kila mwaka, mkurugenzi mkuu wa shirika la kazi duniani ILO, Bwana Guy Ryder anasisitiza changamoto ya kuziba mapengo ya kijamii na kiuchumi ambayo yamejitokeza kutokana na ongezeko la kukosekana kwa usawa.

Amesema wakati dunia imekuwa bora kushikamana kuliko hapo kabla, inaonekana mapengo ya kijamii na kiuchumi yanaongezeka. Mamilioni ya watu wakijihisi wanaachwa nyuma au kuachwa nje kabisa.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “kuzuia migogoro na kudumisha amani kupitia ajira bora” ambapo ILO inataka kuimarishwa kwa usalama na haki katika maeneo ya kazi mathalani nchini Bangladehs ambapo ILO inaimarisha

maizngira ya kazi katika viwanda vya nguo.Tuomo Poutiainen ni Meneja wa mpango wa ILO wa kuboresha viwanda hivyo.

(Sauti Tuomo)

‘‘Kazi halisi ambayo imefanywa ni ujenzi wa tathimini ya usalama, zaidi ya viwanda 5000 vimetathiminiwa, na pia msingi wa taasisi ambayo utasongesha kazi hiyo umeendelezwa. Kazi hii itaendelea katika awamu ya pili lakini sasa kuna uwezo, ujuzi na uelewa kuhusu viwango vya viwanda katika muundo na usalama dhidi ya moto, hayo ni mafanikio makubwa.’’