Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunaweza kutokomeza FGM-WHO

Tunaweza kutokomeza FGM-WHO

Zaidi ya wasichana na wanawake milioni 200 kote duniani ni waathirika wa ukeketaji, mila potofu ambayo Umoja wa Mataifa unasema inazidi kuenezwa kutokana na mwelekeo wa uhamiaji ulimwenguni.

Kufuatia hali hiyo, shirika la afya ulimwenguni, WHO limetumia leo ambayo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukeketaji kuchapisha mwongozo mpya wa kusaidia wataalamu wa afya kukabiliana na FGM wakati huu ambapo ni jambo la kawaida wahudumu wa afya kutekeleza uhalifu huo.

Ian Askew ni mkurugenzi WHO masuala ya afya ya uzazi.

(Sauti ya Askew)

“Ni lazima kufanya kazi nao ili kuwaelimisha maradufu juu ya athari za kuitekeleza hata kama ni kiafya, na pia ni ukiukaji wa haki za binadamu. Ni muhimu kufanya kazi nao na wakuu wa nyanja za kitamaduni na jamii ili waelewe vyema na kutokubali kuzitekeleza ikiwa wataombwa kuzifanya."

Na kuhusu mafanikio ya mpango huo kwingineko, Askew anasema..

(Sauti ya Askew)

“Ndio nchi nyingi tayari zimebuni sheria zenye nguvu zaidi ili kudhibiti utekelezaji wake. Kama unavyofahamu kupitisha sheria na utekelezaji wake huchukua muda. Na tumeanza kuona matokeo katika juhudi ambazo zinatilia mkazo kujumuisha jamii na kujadiliana na familia kwa nini shughuli hii bado inaendelea, faida na ubaya wake.”