Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Niliponea chupu chupu kutoka mikononi mwa Boko Haram

Niliponea chupu chupu kutoka mikononi mwa Boko Haram

Jimbo la Borno nchini Nigeria ni kitovu cha migogoro na janga la kibinadamu linaloletwa na kundi la kigaidi la Boko Haram tangu kuanza kwa mapigano mwaka 2013. Kwa mujibu wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, zaidi ya watu milioni 1.3 wameyakimbia makazi yao na maeneo mengine hayafikiki kutokana na ukatili wao. Katika makala ifuatayo Grace Kaneiya anasimulia madhila aliyoyapitia mmoja wa raia wa eneo hilo ambaye aliweza kutoroka na sasa anatumia kile alichoona kuleta nuru kwa wengine.