Skip to main content

Mahaka ya ICC yawaambia vigogo sita wa Kenya sheria ni msumeno

Mahaka ya ICC yawaambia vigogo sita wa Kenya sheria ni msumeno

Mwendesha mashitaka mkuu wa ICC bwana Luis Moreno Ocampo mapema wiki hii aliamua kumaliza ngojangoja waliyokuwa nayo mamilioni ya Wakenya kutaka kujua ni nani hasa walikuwa vinara wa kuchochea ghasia zilizozuka baada ya uchaguzi mkuu wa Rais Desemba 2007 na mwanzoni mwa 2008 nchini humo.

Watu zaidi ya 1500 waliuawa na wengine maelfu kwa maelfu kulazimika kuzikimbia nyumba zao na kuwa wakimbizi wa ndani. Vigogo sita akiwemo mtangazaji habari wa redio wametajwa.

Nao ni naibu waziri mkuu na waziri wa fedha Uhuru Kenyata, waziri wa viwanda Henry Kosgey, waziri wa zamani wa elimu ya juu William Ruto, kamishina mkuu wa zamani wa polisi Hussein Ali, mwandishi habari wa redio Joshua Sang na mkuu wa utumishi wa umma na katibu katika baraza la mawaziri Francis Muthaura. Mwandishi wetu Jayson Nyakundi amefuatilia kwa karibu sakata hii ungana naye