Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tatizo la ubakaji DRC, ni suruba na adha kwa maelfu ya wanawake, ni lazima likomeshwe:UM

Tatizo la ubakaji DRC, ni suruba na adha kwa maelfu ya wanawake, ni lazima likomeshwe:UM

Wanawake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hususan Kaskazini Mashariki wanaishi wa hofu kubwa kutokana na kushamiri kwa vitendo vya ubakaji.

Katika tarafa ya Fizi wanawake wengi wanaogopa hata kwenda kuteka maji, au kusenya kuni kwani kila kukicha habari zinazoelezwa ni ubakaji unaofanywa na makundi ya wapiganaji wenye silaha.  Mapema mwaka huu Umoja wa Mataifa ulishikia bango serikali ya Congo kuhakikisha hakuna anayetekeleza unyama huo anakwenpa mkono wa sheria.

Mwezi Januari kundi la watu zaidi ya 50 walibakwa na baadhi ya watu wakiwemo wanajeshi, wa jeshi la serikali wakatiwa nguvuni kufuatia ubakaji huo, na 11 kati yao wakakatiwa hukumu vifungo vya kati ya miaka 15 na 30. Idhaa hii imefunga safari hadi vijiji vya Fizi na Atalukulu mkoani Kivu ya Kusini ambako ubakaji wa Januari ulifanyika.

Mwandishi habari Mlolwa Msekke Dide akakutana na baadhi ya kina mama waliobakwa na kumsimulia masahibu yaliyowafika.

(MAKALA NA MSEKE DIDE)