Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umuhimu wa vyoo na huduma za kujisafi

Umuhimu wa vyoo na huduma za kujisafi

Nyumba ni choo! Huu ni usemi ambao hutumika mara nyingi ukiangazia umuhimu wa choo bora na huduma za kujisafi nyumbani.

Tarehe 19 mwezi huu ilikuwa ni siku ya choo duniani.  Dunia imekumbushwa kuwa choo na huduma za kujisafi ambazo hazipewi umuhimu zaweza kuchangia ukuaji wa uchumi.

Umoja wa Mataifa katika taarifa yake umesema maadhimisho ya mwaka huu yana maudhui ya vyoo na ajira na umuhimu wa huduma za kujisafi au ukosefu wake katika ustawi na mazingira ya kazi.

Vyoo vina mchango mkubwa katika kujenga uchumi imara kwani ukosefu wa huduma hizo katika maeneo ya kazi na majumbani una madhara makubwa katika kupunguza uzalishaji.

Takwimu za UM zinaonyesha kuwa asilimia 17 za vifo makazini zinasababishwa na magonjwa ya kuambukiza ikiwemo ukosefu wa vyoo na huduma za kujisafi.

Takwimu hizo pia zinaonyesha kuwa ikiwa huduma hizo zitapewa kipaumbele  uchumi duniani waweza kukuwa kwani dola bilioni 260 zinapotea kila mwaka kwa kukosa huduma za vyoo, usafi na maji safi na salama.

Katika makala yetu ya Wiki tunamulika barani Afrika, hususan ukanda wa maziwa makuu nchini Burundi na mwenyeji wetu ni mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani Kibuga.

(KIBUGA PACKAGE)