Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ebola inaweza kuwa mwokozi wa mafua Afrika:WHO

Ebola inaweza kuwa mwokozi wa mafua Afrika:WHO

Maradhi ya Ebola Afrika ya Magharibi na ukosefu wa chanjo kutibu maradhi hayo yanayouwa, vinaweza kuwa na faida isiyotarajiwa ya kiafya kwa mataifa hayo, ya vita dhidi ya ugonjwa mwingine unaoua wa mafua.

Kwa mujibu wa profesa William Ampofo mshirika wa shirika la afya duniani WHO, wakuu wa nchi za Afrika sasa wameshawishika kuhusu haja ya kutengeneza chanjo katika nchi zao baada ya maradhi ya Ebola kuziyumbisha nchi hizo.

Duniani kote hatua zimepigwa kukabiliana na mafua katika miaka 10 iliyopita, lakini WHO inasema bado ni tishio kubwa linaloendelea kwa maelfu ya watu duniani.