Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpiga picha Mwelu ang’ara tuzo za UNFCU kuhusu SDG’s

Mpiga picha Mwelu ang’ara tuzo za UNFCU kuhusu SDG’s

Julius Mwelu Manyasi mpiaga picha mashuhuri na mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa wa shirika la makazi UN-Habitat Nairobi Kenya, amen’gara kwenye tuzo za kila mwaka za shirikisho la Umoja wa Mataifa la mikopo ( UNFCU )

Tuzo hizo hutokana na shindalo la picha za ubunifu, ambapo washiriki hutakiwa kuwasilisha picha zinazoelezea malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu au SDG’s yanamaanisha nini kwao , mahali wanapofanya kazi au katika jamii zao.

Picha zaidi ya 100 kutoka sehemu mbalimbali duniani zimeshiriki shindalo hilo na Novemba 10 ya Julius Mwelu Manyasi ikaibuka kuwa nambari moja

(JULIUS CUT 1)

Upi ujumbe wake kuhusu SDG’s

(JULIUS CUT 2)

Mshindi wa pili ni Sristi Pradhan kutoka Nepal anayesoma Chuo Kikuu cha New York hapa Marekani huku mpiga picha za sinema kutoka Jamaica Ryan Eccleston ndiye aliyeshikilia nafasi ya tatu.