Skip to main content

Pande zote zina nia ya kudumisha amani Cyprus:Ban

Pande zote zina nia ya kudumisha amani Cyprus:Ban

Viongozi wa pande zote za Cyprus wameanza majadiliano ya wiki nzima Jumatatu ili kupata mustakhbali wa mgawanyiko wa kisiawa hicho, na wanawajibu wa kufanya hivyo ifikapo mwisho wa mwaka huu amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon. Rosemary  Musumba na taarifa kamili.

(TAARIFA YA ROSE)

Akifungua mjadala huo nchini Uswis , Ban ameelezea ni jinsi gani kiongozi wa Cyprus upande wa ugiriki Nicos Anastasiades na yule wa Cyprus ya upande wa Uturuki, Mustafa Akıncı walivyoahidi kufanya kila wawezalo kufikia muafaka mwaka huu 2016.

Hata hivyo Ban ameonya kwamba masauala nyeti na magumu ni lazima tayatuliwe ili kufikia muafaka huo ingawa wamepiga hatua kubwa katika kuelekea kupata suluhu.

Kisiwa hicho cha Mediterraneani kiligawika mapande mawili mwaka 1974 wakati jeshi la Uturuki lilipofanya uvamizi kufuatia jaribio la mapinduzi yaliyoungwa mkono na Ugiriki, na Umoja wa mataifa umekuwa ukijihusisha na ulinzi wa amani Cyprus kwa zaidi ya miaka 50 sasa