Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Getrude abadili mtazamo wa Ukanda wa Ziwa kuhusu mabadiliko ya tabianchi

Getrude abadili mtazamo wa Ukanda wa Ziwa kuhusu mabadiliko ya tabianchi

Nchini Tanzania, mtandao wa wanahabari watoto Tanzania, umeshika hatamu za kuelimisha wananchi kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi, ambapo mmoja wa watoto walioko mstari wa mbele ni Getrude Clement. Getrude ambaye mwezi Aprili mwaka huu alihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kuhusu harakati zake za kutumia picha na radio kuelimisha watu, amemweleza Assumpta Massoi wa Idhaa hii kuwa sasa kiwango cha uelewa kimeongezeka, akitoa mfano jinsi wavuvi kwenye Ziwa Viktoria walivyo mstari wa mbele kukabiliana na magugu maji ambayo yanashambulia mazalia ya samaki. Ametaja pia mipango ya baadaye ikiwemo kusaka maeneo ambayo bado hayajafikiwa lakini yameathirika, lakini kwanza anaanza kwa kuelezea kile alichofanya tangu ahutubie Baraza Kuu.