Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jamii ya kimataifa iongeze shime ya usaidizi CAR- UM

Jamii ya kimataifa iongeze shime ya usaidizi CAR- UM

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mkutano kuhusu utekelezaji wa mamlaka ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA.

Akiwasilisha ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mbele ya wajumbe, Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani katika umoja huo Hervé Ladsous amesema serikali ya CAR kwa usaidizi wa MINUSCA wanaendelea kushirikiana kutekeleza dira ya Rais Faustin-Archange Touadéra kwa mustakhbali wa nchi hiyo.

Dira hiyo ni pamoja na kufanikisha mazungumzo rasmi ya kuzindua mpango wa kitaifa juu ya kupokonya silaha vikundi vilivyojihami na kuwajumuisha katika jamii wapiganaji hao na kuhimiza kuwa….

(Sauti ya Ladsous)

“Ni muhimu kudumisha kasi ya kujenga amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Licha ya maendeleo muhimu yaliyopatikana hadi sasa, taasisi za serikali lazima ziweke bidii bila kuchelewa kuendesha maridhiano ya kitaifa na kufanya marekebisho muhimu katika sekta ya usalama na ulinzi, kukuza na kulinda haki za binadamu na pia kuleta umoja wa kiuchumi maendeleo, kupanua mamlaka chini ya utawala wa sheria, na kuboresha huduma za msingi kwa wote.”

Bwana Ladsous amekariri umuhimu wa wadau kuisaidia nchi hiyo kwenye juhudi zake za kuleta usalama akisema

(Sauti ya Ladsous)

“Kuendelea kwa msaada wa kimataifa ili kusaidia watu Afrika ya Kati katika jitihada zao kwa kuleta amani na utulivu kwa sasa ni muhimu zaidi.”

Amesisitiza pia umuhimu wa mkutano wa Brussels, Ubelgiji wa wafadhili na kimataifa kuhusu CAR utakaofanyika tarehe 17 Novemba akisema kuwa Umoja wa Mataifa utawakilishwa na Naibu Katibu Mkuu.