Skip to main content

Wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu mamluki kufanya ziara CAR

Wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu mamluki kufanya ziara CAR

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu matumizi ya mamluki watatembelea Jamhuri ya Afrika ya Kati kutoka 10 hadi 19 Oktoba mwakahuu ili kukusanya taarifa kuhusu shughuli za mamluki na wapiganaji wa kigeni na ambavyo wamekuwa wakijihusisha katika migogoro ya nchi hiyo.

Pia watatafiti kuhusu wapiganaji hao wa kigeni na athari zake kwa haki za binadamu. Kundi hilo pia litaangalia shughuli za kijeshi na usalama nchini humo. Anton Katz, ambaye anayeongoza kundi hilo akifuatana na mtaalamu mwenzie Patricia Arias amesema wakati wa ziara yao pia watakukutana na wadau mbalimbali ili kujifunza zaidi kuhusu mambo yalivyo, ajira, na athari za mamluki na wapiganaji wa kigeni na kutathimini haki za binadamu, ili waweze kutoa mapendekezo kwa Serikali katika jitihada zake za kujenga nchi upya.

Katika ziara yao watatembelea majimbo ya Bangui, Birao, Bria na Obo. Wataalam hao wapewa jukumu na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kwenda kujifunza na kutambua masuala yanayojitokeza, na mwenendo kuhusu

mamluki na athari zake kwa haki za binadamu. Baada ya ziara hiyo wataanda ripoti watakayoiwasilisha kwenye baraza la haki za binadamu mwaka 2017.