Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna nuru katika kumaliza njaa duniani- Ban

Kuna nuru katika kumaliza njaa duniani- Ban

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewashukuru wakuu wa nchi na serikali kwa kuitikia wito wake tangu mwaka wa 2012 huko mjini Rio de Janeiro alipozindua changamoto ya kumaliza njaa ulimwenguni.

Amesema changamoto hiyo inalenga kuhakikisha kuwa kila mtu anafurahia haki ya msingi ya chakula cha kutosha, dunia ambamo mifumo ya chakula ina umoja, jambo ambalo amesema ni dira ya malengo ya maendeleo endelevu.

Akihutubia mkutano wa viongozi na wadau juu ya kumaliza njaa duniani, Bwana Ban amesema kuwa si haki katika ulimwengu wa sasa karibu watu milioni 800 bado wanakabiliwa na njaa.

Amesema ana imani kuwa pamoja ajenda ya mwaka 2030 kuna nafasi nzuri ya kumaliza njaa na utapiamlo kwa karne hii ambapo amesema tayari ameona maendeleo ya kweli katika miaka minne baada ya uzinduzi huo.

Bwana Ban amesema kwa sasa idadi ya watu duniani watu wenye utapiamlo imeshuka kwa karibu milioni 70 tangu mwaka 2012.