Kutangaza kuwa kura imepigwa bila taarifa za kina hakuleti maana- Mogens

29 Agosti 2016

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limepiga kura isiyo rasmi ikiwa ni mwelekeo wake wa kuchuja wagombea nafasi ya ukatibu mkuu wa umoja huo.

Ingawa matokeo hayajatangazwa, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Mogens Lykettoft amesema amearifiwa na Rais wa Baraza la Usalama balozi Ramlan bin Ibrahim wa Malaysia juu ya kufanyika kwa kura hiyo ikiwa ni awamu ya tatu, baada ya awamu mbili za awali.

Katika taarifa yake Mogens amesema amweleza tena Balozi Ibrahim kuwa pamoja na kutambua mantiki nzima ya kura hiyo kutokuwa rasmi, bado anasisitiza kuwa ukosefu wa taarifa nyingine zaidi ya kwamba kura hiyo imefanyika, haiongezi thamani yoyote kwa matarajio ya wanachama na viwango vipya ya uwazi katika mchakato huo.

Awali jumla ya wagombea 12 walikuwa wamejitokeza lakini idadi hiyo imepungua hadi 10 baada ya wagombea wawili kujitoa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter